2 Kings 13:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nabii Elisha aliugua ugonjwa mbaya sana. Alipokuwa karibu kufa, mfalme Yehoashi wa Israeli alimtembelea. Alipomfikia Elisha, alilia, akisema, “Baba yangu, baba yangu! Magari ya Israeli na wapandafarasi wake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huu, Al-Yasa alikuwa anaugua ugonjwa ambao baadaye ulimuua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nabii Elisha aliugua ugonjwa mbaya sana. Alipokuwa karibu kufa, mfalme Yehoashi wa Israeli alimtembelea. Alipomfikia Elisha, alilia, akisema, “Baba yangu, baba yangu! Magari ya Israeli na wapandafarasi wake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huu, Elisha alikuwa anaumwa na ugonjwa ambao baadaye ulimwua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huu, Al-Yasa alikuwa anaumwa na ugonjwa ambao baadaye ulimuua. Yehoashi mfalme wa Israeli akashuka kwenda kumwona na kumlilia. Akalia, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya vita ya Israeli na wapanda farasi wake!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nabii Elisha aliugua ugonjwa mbaya sana. Alipokuwa karibu kufa, mfalme Yehoashi wa Israeli alimtembelea. Alipomfikia Elisha, alilia, akisema, “Baba yangu, baba yangu! Magari ya Israeli na wapandafarasi wake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elisa alipopata ugonjwa wake uliomwua, ndipo, Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, aliposhuka kuja kwake, akalia machozi mbele yake na kusema: Baba yangu! Baba yangu! Wewe gari la Waisiraeli na wapanda farasi wake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nabii Elisha alipata ugonjwa ambao ulimwua. Alipokuwa karibu kufa, mufalme Yehoasi wa Israeli alimutembelea. Alipomufikia Elisha, akalia, akisema: “Baba yangu, baba yangu! Ulikuwa wa lazima kuliko magari ya Israeli na wapanda-farasi wake!”