2 Kings 13:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mmoja, wakati wa mazishi, watu waliona kundi mojawapo la watu waliobeba maiti wakamtupa yule maiti kaburini mwa Elisha na kukimbia. Mara maiti huyo alipogusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama wima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Al-Yasa. Ile maiti ilipogusa mifupa ya Al-Yasa, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mmoja, wakati wa mazishi, watu waliona kundi mojawapo la watu waliobeba maiti wakamtupa yule maiti kaburini mwa Elisha na kukimbia. Mara maiti huyo alipogusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama wima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Elisha. Wakati ile maiti ilipogusa mifupa ya Elisha, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa Waisraeli fulani walipokuwa wanamzika mtu, ghafula wakaona kikosi cha washambuliaji, basi wakaitupa ile maiti ya yule mtu ndani ya kaburi la Al-Yasa. Wakati ile maiti ilipogusa mifupa ya Al-Yasa, yule mtu akafufuka na kusimama kwa miguu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mmoja, wakati wa mazishi, watu waliona kundi mojawapo la watu waliobeba maiti wakamtupa yule maiti kaburini mwa Elisha na kukimbia. Mara maiti huyo alipogusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama wima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, walipotoka, waende kuzika mtu, mara wakaona kikosi; kwa hiyo wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisa. Lakini yule mtu alipofika ndani na kuigusa mifupa ya Elisa, mara akawa mzima tena, akaweza kusimama miguuni pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, wakati wa mazishi, watu waliona moja kati ya makundi yale. Wakatupa maiti katika kaburi la Elisha na kukimbia. Mara tu maiti hiyo ilipogusa mifupa ya Elisha, ilifufuka na kusimama wima.