2 Kings 13:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Mwenyezi-Mungu akawapa watu wa Israeli kiongozi ambaye aliwakomboa kutoka kwa Washamu, ndipo wakakaa kwa amani kama vile walivyokuwa hapo awali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(Bwana akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Mwenyezi-Mungu akawapa watu wa Israeli kiongozi ambaye aliwakomboa kutoka kwa Washamu, ndipo wakakaa kwa amani kama vile walivyokuwa hapo awali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka kwenye mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akamtoa mwokozi kwa ajili ya Israeli, nao wakaokoka kutoka kwenye mamlaka ya Aramu. Hivyo Waisraeli wakaishi katika nyumba zao wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(BWANA akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Mwenyezi-Mungu akawapa watu wa Israeli kiongozi ambaye aliwakomboa kutoka kwa Washamu, ndipo wakakaa kwa amani kama vile walivyokuwa hapo awali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipowapa Waisiraeli mwokozi, wakatoka mikononi mwa Washami, wana wa Isiraeli wakapata kukaa tena mahemani kwao kama huko kale,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(BWANA akawapa Israeli mwokozi, nao wakatoka mikononi mwa Washami; wana wa Israeli wakakaa hemani mwao kama zamani za kwanza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akawapa Waisraeli kiongozi ambaye aliwakomboa kutoka kwa Waaramu. Halafu wakakaa kwa amani kama vile walivyokuwa zamani.