2 Kings 14:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehoashi mfalme wa Israeli alimteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yehoashi, mwana wa Ahazia huko Beth-shemeshi; halafu akauendea Yerusalemu na kuubomoa ukuta wake kutoka Lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, umbali wa karibu mita 200.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoashi mfalme wa Israeli akamteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akaenda Yerusalemu na kuubomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi Lango la Pembeni, sehemu yenye urefu wa kama dhiraa mia nne.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwanawe Yoashi mwana wa Ahazia, huko Beth-shemeshi, akaja Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu toka lango la Efraimu hata lango la pembeni, mikono mia nne.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehoashi mfalme wa Israeli alimteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yehoashi, mwana wa Ahazia huko Beth-shemeshi; halafu akauendea Yerusalemu na kuubomoa ukuta wake kutoka Lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, umbali wa karibu mita 200.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoashi mfalme wa Israeli akamkamata Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akaenda Yerusalemu na kuvunja ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi Lango la Kwenye Pembe, kisehemu chenye urefu wa kama dhiraa 400.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoashi mfalme wa Israeli akamteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yoashi, mwana wa Ahazia, huko Beth-Shemeshi. Kisha Yehoashi akaenda Yerusalemu na kuubomoa ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi Lango la Pembeni, sehemu yenye urefu wa kama dhiraa 400.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwanawe Yoashi mwana wa Ahazia, huko Beth-shemeshi, akaja Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu toka lango la Efraimu hata lango la pembeni, dhiraa mia nne.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehoashi mfalme wa Israeli alimteka Amazia mfalme wa Yuda, mwana wa Yehoashi, mwana wa Ahazia huko Beth-shemeshi; halafu akauendea Yerusalemu na kuubomoa ukuta wake kutoka Lango la Efraimu mpaka Lango la Pembeni, umbali wa karibu mita 200.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yoasi, mfalme wa Waisiraeli, akamkamata Amasia, mfalme wa Wayuda, aliyekuwa mwana wa Yoasi, mwana wa Yoahazi, kule Beti-Semesi, kisha akaja Yerusalemu, akalivunja boma la Yerusalemu toka lango la Efuraimu hata lango la pembeni, ndio mikono 400.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yehoashi mfalme wa Israeli akamtwaa Amazia mfalme wa Yuda, mwanawe Yoashi mwana wa Ahazia, huko Beth-shemeshi, akaja Yerusalemu, akauvunja ukuta wa Yerusalemu toka lango la Efraimu hata lango la pembeni, mikono mia nne.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoasi mufalme wa Israeli alimuteka Amazia mufalme wa Yuda mwana wa Yoasi mwana wa Ahazia kule Beti-Semesi. Halafu akauendea Yerusalema na kuubomoa ukuta wake kutoka kwenye Mulango wa Efuraimu mpaka kwenye Mulango wa Pembeni, umbali wa karibu metre mia mbili.