2 Kings 14:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo mengine yote ya Yeroboamu, vita alivyopigana kwa ushujaa, na jinsi alivyoikomboa Damasko na Hamathi na kuifanya mali ya Israeli, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, yote aliyoyafanya na mafanikio yake ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na jinsi alivyorudisha Dameski na Hamathi kwa Israeli, ambayo ilikuwa mali ya Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mambo yote ya Yeroboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, na jinsi aliyvopigana, akawapatia tena Israeli Dameski na Hamathi, iliyokuwa kwanza ya Yuda, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo mengine yote ya Yeroboamu, vita alivyopigana kwa ushujaa, na jinsi alivyoikomboa Damasko na Hamathi na kuifanya mali ya Israeli, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, yote aliyoyafanya na mafanikio yake ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na jinsi alivyorudisha Dameski na Hamathi kwa Israeli, ambayo ilikuwa mali ya Yaudi, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Israeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa matukio mengine ya utawala wa Yeroboamu, yote aliyoyafanya na mafanikio yake ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na jinsi alivyorudisha Dameski na Hamathi kwa Israeli, ambayo ilikuwa mali ya Yuda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mambo yote ya Yeroboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, na jinsi alivyopigana, akawapatia tena Israeli Dameski na Hamathi, iliyokuwa kwanza ya Yuda, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matendo mengine yote ya Yeroboamu, vita alivyopigana kwa ushujaa, na jinsi alivyoikomboa Damasko na Hamathi na kuifanya mali ya Israeli, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo mengine ya Yeroboamu, nayo yote, aliyoyafanya, na matendo yake yaliyokuwa yenye nguvu, alipopiga vita, tena jinsi alivyoirudisha kwa Waisiraeli miji ya Damasko na ya Hamati iliyokuwa kale ya Wayuda, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Waisiraeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mambo yote ya Yeroboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, na jinsi aliyvopigana, akawapatia tena Israeli Dameski na Hamathi, iliyokuwa kwanza ya Yuda, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo mengine ya Yeroboamu, yote aliyofanya, vita alivyopigana kwa ushujaa, na jinsi alivyoikomboa Damasiki na Hamati na kuifanya mali ya Israeli, yote yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Siku za Wafalme wa Israeli.