2 Kings 14:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu Amazia alipojiimarisha mamlakani, aliwaua watumishi waliomuua mfalme, baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya ufalme kuimarika mkononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, mara ufalme ulipokuwa imara mkononi mwake, aliwaua watumishi wale waliomwua mfalme baba yake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu Amazia alipojiimarisha mamlakani, aliwaua watumishi waliomuua mfalme, baba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya ufalme kuwa imara mikononi mwake, aliwaua wale maafisa waliomwua Mfalme Yoashi baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya ufalme kuimarika mikononi mwake, aliwaua maafisa waliomuua mfalme baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, mara ufalme ulipokuwa imara mkononi mwake, aliwaua watumishi wale waliomwua mfalme baba yake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu Amazia alipojiimarisha mamlakani, aliwaua watumishi waliomuua mfalme, baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, ufalme ulipopata kushupaa mkononi mwake, akawaua watumishi wake waliomwua baba yake mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, mara ufalme ulipokuwa imara mkononi mwake, aliwaua watumishi wale waliomwua mfalme baba yake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Amazia alipojiimarisha katika mamlaka, aliwaua watumishi waliomwua mufalme baba yake.