2 Kings 15:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Peka mwana wa Remalia, ambaye alikuwa ofisa wa jeshi la Pekahia, alishirikiana na watu wengine hamsini kutoka Gileadi, akamuua Pekahia katika ngome ya ndani ya nyumba ya mfalme huko Samaria, na kuwa mfalme mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akapanga njama dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamuua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamuua Pekahia, naye akawa mfalme baada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia fitina, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Peka mwana wa Remalia, ambaye alikuwa ofisa wa jeshi la Pekahia, alishirikiana na watu wengine hamsini kutoka Gileadi, akamuua Pekahia katika ngome ya ndani ya nyumba ya mfalme huko Samaria, na kuwa mfalme mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akafanya shauri baya dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamwua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamwua Pekahia, naye akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wa maafisa wake wakuu, Peka mwana wa Remalia, akafanya shauri baya dhidi yake. Akachukua watu hamsini wa Gileadi pamoja naye, akamuua Pekahia, pamoja na Argobu na Aria, katika ngome ya jumba la kifalme huko Samaria. Kwa hiyo Peka akamuua Pekahia, naye akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia uhaini, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Peka mwana wa Remalia, ambaye alikuwa ofisa wa jeshi la Pekahia, alishirikiana na watu wengine hamsini kutoka Gileadi, akamuua Pekahia katika ngome ya ndani ya nyumba ya mfalme huko Samaria, na kuwa mfalme mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Peka, mwana wa Remalia, mkuu wake wa askari 30 akamlia njama, akamwua pamoja na Argobu na Arie huko Samaria katika jumba kubwa lililokuwa nyumba ya mfalme, hata watu 50 wa wana wa Gileadi walikuwa naye. Alipokwisha kumwua akawa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia fitina, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Peka mwana wa Remalia, ambaye alikuwa mukubwa wa waaskari wa Pekahia, alishirikiana na watu wengine makumi tano kutoka Gileadi, akamwua Pekahia katika chumba cha ndani cha nyumba ya mufalme kule Samaria na kuwa mufalme kwa pahali pake.