2 Kings 15:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa enzi ya mfalme Azaria wa Yuda, Peka mwana wa Remalia alianza kutawala huko Samaria, akatawala kwa muda wa miaka ishirini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa enzi ya mfalme Azaria wa Yuda, Peka mwana wa Remalia alianza kutawala huko Samaria, akatawala kwa muda wa miaka ishirini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa kutawala kwake Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akawa mfalme wa Israeli huko Samaria, naye alitawala miaka ishirini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa enzi ya mfalme Azaria wa Yuda, Peka mwana wa Remalia alianza kutawala huko Samaria, akatawala kwa muda wa miaka ishirini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa 52 wa Azaria, mfalme wa Wayuda, Peka, mwana wa Remalia, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli mle Samaria miaka 20.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa makumi tano na mbili wa utawala wa mufalme Azaria wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala akiwa kule Samaria kwa muda wa miaka makumi mbili.