2 Kings 15:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Azaria alifariki na kuzikwa katika makaburi ya wafalme katika mji wa Daudi; na mwanawe Yothamu alitawala mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Azaria akalala na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi. Naye Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Azaria alifariki na kuzikwa katika makaburi ya wafalme katika mji wa Daudi; na mwanawe Yothamu alitawala mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Azaria akalala pamoja na baba zake naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi, na Yothamu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Azaria akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika Mji wa Daudi, na Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Azaria alifariki na kuzikwa katika makaburi ya wafalme katika mji wa Daudi; na mwanawe Yothamu alitawala mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Azaria alipokwenda kulala na baba zake, wakamzika kwa baba zake mjini mwa Dawidi, naye mwanawe Yotamu akawa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Azaria akakufa na kuzikwa katika makaburi ya wafalme katika muji wa Daudi; na mwana wake Yotamu akatawala kwa pahali pake.