2 Kings 16:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Ahazi alipokwenda Damasko kukutana na mfalme Tiglath-pileseri, aliona madhabahu huko. Basi, akamtumia kuhani Uria mfano kamili na mchoro wa madhabahu hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaona madhabahu huko Dameski, naye akamtumia Uria kuhani mchoro wa hayo madhabahu, pamoja na maelezo ya mpango kamili wa ujenzi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Ahazi alipokwenda Damasko kukutana na mfalme Tiglath-pileseri, aliona madhabahu huko. Basi, akamtumia kuhani Uria mfano kamili na mchoro wa madhabahu hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaiona madhabahu huko Dameski na akamtumia Uria kuhani mchoro wa hiyo madhabahu, pamoja na maelezo yakiwa ya mpango kamili kwa ajili ya ujenzi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Mfalme Ahazi akaenda Dameski kukutana na Tiglath-Pileseri wa Ashuru. Akaona madhabahu huko Dameski, naye akamtumia Uria kuhani mchoro wa hayo madhabahu, pamoja na maelezo ya mpango kamili wa ujenzi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Ahazi alipokwenda Damasko kukutana na mfalme Tiglath-pileseri, aliona madhabahu huko. Basi, akamtumia kuhani Uria mfano kamili na mchoro wa madhabahu hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme Ahazi akaenda Damasko kuonana na Tiglati-Pileseri, mfalme wa Asuri. Alipoiona meza ya kutambikia iliyoko Damasko mfalme Ahazi akatuma mfano wa hiyo meza ya kutambikia kuionyesha namna yake, ilivyotengenezwa kazi zake zote, akaupeleka kwa mtambikaji Uria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Ahazi alipokwenda Damasiki kukutana na mufalme Tigilati-Pileseri, aliona mazabahu kule. Basi, akamutumia kuhani Uria mufano kamili na muchoro wa mazabahu hiyo.