2 Kings 16:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Madhabahu ya shaba ambayo iliwekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, aliiondoa mbele ya nyumba kutoka nafasi yake katikati ya madhabahu yake na nyumba ya Mwenyezi-Mungu, akaiweka kwenye nafasi iliyokuwa upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme Ahazi akayaondoa madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, yaliyokuwa yamesimama kati ya ingilio la Hekalu na hayo madhabahu mapya, naye akayaweka upande wa kaskazini mwa hayo madhabahu mapya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ile madhabahu ya shaba iliyokuwako mbele za Bwana, akaileta kutoka mbele ya nyumba, kutoka kati ya madhabahu yake mwenyewe na nyumba ya Bwana, akaiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Madhabahu ya shaba ambayo iliwekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, aliiondoa mbele ya nyumba kutoka nafasi yake katikati ya madhabahu yake na nyumba ya Mwenyezi-Mungu, akaiweka kwenye nafasi iliyokuwa upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Ahazi akaiondoa ile madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la BWANA, iliyokuwa imesimama kati ya ingilio la Hekalu na hiyo madhabahu mpya, naye akaiweka upande wa kaskazini mwa hiyo madhabahu mpya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Ahazi akayaondoa madhabahu ya zamani ya shaba kutoka hapo mbele ya Hekalu la bwana, yaliyokuwa yamesimama kati ya ingilio la Hekalu na hayo madhabahu mapya, naye akayaweka upande wa kaskazini mwa hayo madhabahu mapya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ile madhabahu ya shaba iliyokuwako mbele za BWANA, akaileta kutoka mbele ya nyumba, kutoka kati ya madhabahu yake mwenyewe na nyumba ya BWANA, akaiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Madhabahu ya shaba ambayo iliwekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, aliiondoa mbele ya nyumba kutoka nafasi yake katikati ya madhabahu yake na nyumba ya Mwenyezi-Mungu, akaiweka kwenye nafasi iliyokuwa upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo ile meza ya shaba ya kutambikia iliyokuwako mbele ya Bwana akaiondoa mahali pake mbele ya Nyumba, isiwe tena katikati ya hiyo meza mpya ya kutambikia na Nyumba ya Bwana, akaiweka upande wa kaskazini wa hiyo meza mpya ya kutambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ile madhabahu ya shaba iliyokuwako mbele za BWANA, akaileta kutoka mbele ya nyumba, kutoka kati ya madhabahu yake mwenyewe na nyumba ya BWANA, akaiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazabahu ya shaba ambayo ilitakaswa kwa ajili ya Yawe, aliiondoa mbele ya nyumba kutoka nafasi yake katikati ya mazabahu yake na nyumba ya Yawe, akaiweka kwenye nafasi iliyokuwa upande wa kaskazini wa mazabahu yake.