2 Kings 16:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali alifuata mienendo ya wafalme wa Israeli. Isitoshe, hata alimpitisha mwanawe motoni kuwa tambiko, akifuata desturi mbaya za mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na hata akamtoa kafara mwanawe katika moto, akifuata njia za machukizo za mataifa ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali alifuata mienendo ya wafalme wa Israeli. Isitoshe, hata alimpitisha mwanawe motoni kuwa tambiko, akifuata desturi mbaya za mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli na hata kumtoa mwanawe kafara katika moto, akafuata njia za machukizo za mataifa ambayo BWANA alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, na hata akamtoa mwanawe kafara katika moto, akifuata njia za machukizo za mataifa ambayo bwana alikuwa ameyafukuza mbele ya Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali alifuata mienendo ya wafalme wa Israeli. Isitoshe, hata alimpitisha mwanawe motoni kuwa tambiko, akifuata desturi mbaya za mataifa ambayo yalifukuzwa na Mwenyezi-Mungu Waisraeli walipokuwa wanaingia nchini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila akaendelea kuzishika njia za wafalme wa Waisiraeli, hata mwanawe akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa motoni akiyafuata hayo matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele yao Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini alifuata mwenendo wa wafalme wa Israeli. Akamutambikia hata mwana wake kwa kuteketezwa kwa moto, akifuata desturi mbaya za mataifa ambayo yalifukuzwa na Yawe wakati Waisraeli walipokuwa wanaingia katika inchi.