2 Kings 17:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walikataa kutii maagizo yake; hawakushika agano alilofanya na babu zao; licha ya kupuuza maonyo yake, waliabudu sanamu zisizokuwa na maana mpaka hata wao wenyewe hawakuwa na maana tena; walifuata desturi za mataifa yaliyowazunguka: Walipuuza amri za Mwenyezi-Mungu; wala hawakuzizingatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walizikataa amri zake, na agano alilolifanya na baba zao, na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu batili, nao wenyewe wakawa batili. Wakayaiga mataifa yaliyowazunguka, ingawa Mwenyezi Mungu alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao Bwana alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walikataa kutii maagizo yake; hawakushika agano alilofanya na babu zao; licha ya kupuuza maonyo yake, waliabudu sanamu zisizokuwa na maana mpaka hata wao wenyewe hawakuwa na maana tena; walifuata desturi za mataifa yaliyowazunguka: walipuuza amri za Mwenyezi-Mungu; wala hawakuzizingatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walizikataa amri zake na Agano alilokuwa amelifanya na baba zao na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. Wakayaigiza mataifa yaliyowazunguka, ingawa BWANA alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya,” nao wakafanya mambo ambayo BWANA alikuwa amewakataza wasifanye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walizikataa amri zake, na agano alilokuwa amelifanya na baba zao, na maonyo aliyokuwa amewapa. Wakafuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. Wakayaiga mataifa yaliyowazunguka, ingawa bwana alikuwa amewaonya akiwaambia, “Msifanye kama wanavyofanya,” nao wakafanya mambo ambayo bwana alikuwa amewakataza wasifanye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walikataa kutii maagizo yake; hawakushika agano alilofanya na babu zao; licha ya kupuuza maonyo yake, waliabudu sanamu zisizokuwa na maana mpaka hata wao wenyewe hawakuwa na maana tena; walifuata desturi za mataifa yaliyowazunguka: Walipuuza amri za Mwenyezi-Mungu; wala hawakuzizingatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakayakataa maongozi yake na Agano lake, aliloliagana na baba zao, nao ushuhuda wake, aliowashuhudia, wakafuata mambo yasiyo na maana wakifanya yaliyo ya bure kabisa, wakawafuata wamizimu waliokaa na kuwazunguka pande zote, naye Bwana alikuwa amewaagiza, wasifanye kama wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walikataa kutii masharti yake; hawakushika agano alilofanya na babu zao, walizarau maonyo yake, waliabudu sanamu zisizokuwa na maana hata wao wenyewe hawakukuwa na maana tena, walifuata desturi za mataifa yaliyowazunguka: walizarau amri za Yawe; wala hawakuzishika.