2 Kings 17:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walivunja amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakatengeneza sanamu za miungu ya ndama wawili wa kusubu; vilevile wakatengeneza sanamu za mungu wa kike Ashera wakaabudu na vitu vyote vya angani na wakamtumikia Baali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakayaacha maagizo yote ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kujitengenezea sanamu mbili, walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, na wakamtumikia Baali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaziacha amri zote za Bwana, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walivunja amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakatengeneza sanamu za miungu ya ndama wawili wa kusubu; vilevile wakatengeneza sanamu za mungu wa kike Ashera wakaabudu na vitu vyote vya angani na wakamtumikia Baali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakayaacha maagizo yote ya BWANA Mungu wao na kujitengenezea sanamu mbili walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, wakamtumikia Baali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakayaacha maagizo yote ya bwana Mwenyezi Mungu wao na kujitengenezea sanamu mbili, walizozisubu katika sura ya ndama na nguzo ya Ashera. Wakasujudia mianga yote ya angani, na wakamtumikia Baali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wakajitengenezea sanamu za kusubu, yaani, ndama wawili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walivunja amri zote za Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, wakatengeneza sanamu za miungu ya ndama wawili wa kusubu; vilevile wakatengeneza sanamu za mungu wa kike Ashera wakaabudu na vitu vyote vya angani na wakamtumikia Baali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakayaacha maagizo yote ya Bwana Mungu wao, wakajitengenezea vinyago viwili vya ndama kwa shaba zilizoyeyushwa, tena wakajitengenezea vinyago vya Ashera, wakaviangukia navyo vikosi vyote vya mbinguni, wakamtumikia hata Baali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walivunja amri zote za Yawe, Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za miungu ya wana-ngombe wawili wa madini yenye kuyeyushwa, wakatengeneza sanamu za Ashera, wakaabudu jeshi la mbingu, na wakamutumikia Bali.