2 Kings 17:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliwatambika watoto wao wa kiume na wa kike kwa miungu ya uongo; wakataka shauri kwa watabiri na wachawi. Walinuia kabisa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakamkasirisha sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakawatoa kafara watoto wao wa kiume na wa kike katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa Mwenyezi Mungu, wakamghadhibisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliwatambika watoto wao wa kiume na wa kike kwa miungu ya uongo; wakataka shauri kwa watabiri na wachawi. Walinuia kabisa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakamkasirisha sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakawatoa kafara wana wao na mabinti zao katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa BWANA, wakamghadhibisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakawatoa kafara wana wao na mabinti zao katika moto. Wakafanya uaguzi na uchawi, nao wakajiuza wenyewe katika kutenda uovu machoni pa bwana, wakamghadhibisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakawapitisha watoto wao, wa kiume na wa kike, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza wenyewe wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliwatambika watoto wao wa kiume na wa kike kwa miungu ya uongo; wakataka shauri kwa watabiri na wachawi. Walinuia kabisa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakamkasirisha sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata wana wao wa kiume na wa kike wakawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni, wakaagua maaguaji kwa kutabana, wakajiuza katika utumwa wa kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wamkasirishe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliwatambikia watoto wao wa kiume na wa kike kwa miungu ya uongo; wakaomba shauri kwa watabiri na wachawi. Walijitoa kabisa kutenda maovu mbele ya Yawe, wakamukasirikisha sana.