2 Kings 17:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme wa Ashuru akachukua watu kutoka Babuloni, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria mahali pa watu wa Israeli waliopelekwa uhamishoni. Wakaitwaa miji hiyo na kukaa humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme wa Ashuru akachukua watu kutoka Babuloni, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria mahali pa watu wa Israeli waliopelekwa uhamishoni. Wakaitwaa miji hiyo na kukaa humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria badala ya Waisraeli. Wakaimiliki Samaria na kuishi katika miji yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme wa Ashuru akachukua watu kutoka Babuloni, Kutha, Ava, Hamathi na Sefarvaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria mahali pa watu wa Israeli waliopelekwa uhamishoni. Wakaitwaa miji hiyo na kukaa humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme wa Asuri akatoa watu mle Babeli na Kuta na Awa na Hamati na Sefarwaimu, akawakalisha katika miji ya Samaria mahali pao wana wa Isiraeli, wakaitwaa nchi ya Samaria, iwe yao, wakakaa katika miji yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme wa Asuria akapeleka watu kutoka Babeli, Kuta, Awa, Hamati na Sefarwaimu na kuwaweka katika miji ya Samaria kwa pahali pa watu wa Israeli waliopelekwa katika uhamisho. Wakaitwaa miji hiyo na kukaa mule.