2 Kings 17:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya agano nao na kuwaamuru, “Msiabudu miungu mingine; msiisujudie, msiitumikie wala msiitambikie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli, aliwaamuru: “Msiiabudu miungu mingine yoyote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hao ambao Bwana alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya agano nao na kuwaamuru, “Msiabudu miungu mingine; msiisujudie, msiitumikie wala msiitambikie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati BWANA alipofanya Agano na Waisraeli aliwaamuru akisema: “Msiiabudu miungu mingine yo yote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati bwana alipofanya Agano na Waisraeli, aliwaamuru akisema: “Msiiabudu miungu mingine yoyote wala kuisujudia, wala kuitumikia wala kuitolea dhabihu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hao ambao BWANA alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alikuwa amefanya agano nao na kuwaamuru, “Msiabudu miungu mingine; msiisujudie, msiitumikie wala msiitambikie.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bwana alikuwa amefanya agano nao na kuwaagiza kwamba: Msiche miungu mingine, wala msiiangukie, wala msiitumikie, wala msiitambikie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hao ambao BWANA alifanya agano nao, akawaamuru, akasema, Msiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuitumikia, wala kuitolea sadaka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alikuwa amefanya agano nao na kuwaamuru: “Musiabudu miungu mingine; musiiname mbele yake, musiitumikie wala musiitambikie.