2 Kings 17:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi mataifa haya yalimwabudu Mwenyezi-Mungu, lakini pia yalitumikia sanamu zao za kusubu; na mpaka sasa hivi, wazawa wao wanaendelea kutenda hivyo kama walivyotenda babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata wakati watu hawa walipokuwa wanamwabudu Mwenyezi Mungu, walikuwa bado wakitumikia sanamu zao. Hadi leo watoto wao na wajukuu wao wanaendelea kufanya kama baba zao walivyofanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mataifa hawa wakamcha Bwana, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi mataifa haya yalimwabudu Mwenyezi-Mungu, lakini pia yalitumikia sanamu zao za kusubu; na mpaka sasa hivi, wazawa wao wanaendelea kutenda hivyo kama walivyotenda babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata wakati watu hawa walipokuwa wanamwabudu BWANA, walikuwa bado wakitumikia sanamu zao. Mpaka leo watoto wao na watoto wa watoto wao wanaendelea kufanya kama baba zao walivyofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata wakati watu hawa walipokuwa wanamwabudu bwana, walikuwa bado wakitumikia sanamu zao. Mpaka leo watoto wao na watoto wa watoto wao wanaendelea kufanya kama baba zao walivyofanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mataifa hawa wakamcha BWANA, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi mataifa haya yalimwabudu Mwenyezi-Mungu, lakini pia yalitumikia sanamu zao za kusubu; na mpaka sasa hivi, wazawa wao wanaendelea kutenda hivyo kama walivyotenda babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, hao wamizimu walivyomcha Bwana pamoja na kuvitumikia vinyago vyao. Hata wana wao na wana wa wana wao wakayafanya mpaka siku hii ya leo, kama baba zao walivyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mataifa hawa wakamcha BWANA, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mataifa haya yalimwabudu Yawe, lakini vilevile walitumikia sanamu zao za madini yenye kuyeyushwa; na mpaka sasa hivi, wazao wao wanaendelea kutenda hivyo kama vile babu zao walivyotenda.