2 Kings 17:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Haya yote yalitendeka kwa sababu watu wa Israeli walimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, ambaye aliwatoa kutoka mikononi mwa mfalme wa Misri, pia waliabudu miungu mingine,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yote haya yalitukia kwa sababu Waisraeli walikuwa wametenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, aliyekuwa amewapandisha kutoka Misri akiwatoa chini ya utawala wa nguvu wa Farao mfalme wa Misri. Waliabudu miungu mingine,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya Bwana, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Haya yote yalitendeka kwa sababu watu wa Israeli walimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, ambaye aliwatoa kutoka mikononi mwa mfalme wa Misri, pia waliabudu miungu mingine,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yote haya yalitokea kwa sababu Waisraeli walikuwa wametenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wao, ambaye alikuwa amewapandisha kutoka Misri akiwatoa chini ya utawala wa nguvu wa Farao mfalme wa Misri. Waliabudu miungu mingine
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yote haya yalitokea kwa sababu Waisraeli walikuwa wametenda dhambi dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wao, ambaye alikuwa amewapandisha kutoka Misri akiwatoa chini ya utawala wa nguvu wa Farao mfalme wa Misri. Waliabudu miungu mingine
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya BWANA, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakaiacha miungu mingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Haya yote yalitendeka kwa sababu watu wa Israeli walimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, ambaye aliwatoa kutoka mikononi mwa mfalme wa Misri, pia waliabudu miungu mingine,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa hivyo, kwa kuwa wana wa Isiraeli walimkosea Bwana Mungu wao aliyewatoa utumwani katika nchi ya Misri mkononi mwa Farao, mfalme wa Misri, lakini wao wakacha miungu mingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya BWANA, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya yote yalitendeka kwa sababu watu wa Israeli walimwasi Yawe, Mungu wao, ambaye aliwatoa kutoka mikono ya mufalme wa Misri, vilevile waliabudu miungu mingine,