2 Kings 17:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye ngome, walijijengea mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya BWANA Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye maboma walijijengea wenyewe mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli wakafanya vitu kwa siri dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wao, ambavyo havikuwa sawa. Kuanzia kwenye mnara wa ulinzi hadi kwenye mji wenye maboma walijijengea wenyewe mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji yao yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walijenga mahali pa juu pa kuabudia miungu ya uongo katika kila mji, kuanzia mnara wa walinzi mashambani hadi katika mji wenye ngome.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo wana wa Isiraeli walimkosea Bwana Mungu wao na kufanya mafichoni mambo yasiyopasa kuyafanya, wakijijengea pa kutambikia vilimani katika miji yao yote iliyokuwa yenye minara tu ya kungojea, namo mijini mlimo na maboma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya BWANA, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Israeli walitenda kwa siri mambo yasiyokuwa mema mbele za Yawe, Mungu wao. Walijenga nafasi ya kuabudu miungu ya uongo katika kila muji, kuanzia kwenye munara wa walinzi katika mashamba mpaka katika miji yenye kuta.