2 Kings 18:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hezekia akatuma ujumbe kwa Senakeribu huko Lakishi na kumwambia, “Nimefanya makosa. Tafadhali, komesha mashambulio yako kwangu; nami nitalipa chochote utakacho.” Mfalme wa Ashuru akaagiza Hezekia amletee tani kumi za fedha na tani moja ya dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa chochote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta mia tatu za fedha, na talanta thelathini za dhahabu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Hezekia, mfalme wa Yuda, akapeleka wajumbe waende Lakishi kwa mfalme wa Ashuru, kusema, Nimekosa; uniache ukarudi kwako; cho chote utakachoweka juu yangu, nitakichukua. Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia, mfalme wa Yuda, talanta za fedha mia tatu, na talanta za dhahabu thelathini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hezekia akatuma ujumbe kwa Senakeribu huko Lakishi na kumwambia, “Nimefanya makosa. Tafadhali, komesha mashambulio yako kwangu; nami nitalipa chochote utakacho.” Mfalme wa Ashuru akaagiza Hezekia amletee tani kumi za fedha na tani moja ya dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa cho chote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta 300 za fedha na talanta thelathini za dhahabu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Hezekia mfalme wa Yuda akamtumia ujumbe mfalme wa Ashuru huko Lakishi akisema: “Nimefanya makosa. Ondoka katika nchi yangu, nami nitakulipa chochote unachokitaka kwangu.” Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia mfalme wa Yuda talanta 300 za fedha, na talanta thelathini za dhahabu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Hezekia, mfalme wa Yuda, akapeleka wajumbe waende Lakishi kwa mfalme wa Ashuru, kusema, Nimekosa; uniache ukarudi kwako; chochote utakachoweka juu yangu, nitakichukua. Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia, mfalme wa Yuda, talanta za fedha mia tatu, na talanta za dhahabu thelathini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hezekia akatuma ujumbe kwa Senakeribu huko Lakishi na kumwambia, “Nimefanya makosa. Tafadhali, komesha mashambulio yako kwangu; nami nitalipa chochote utakacho.” Mfalme wa Ashuru akaagiza Hezekia amletee tani kumi za fedha na tani moja ya dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Hizikia, mfalme wa Wayuda, akatuma Lakisi kwa mfalme wa Asuri kumwambia: Nimekosa, ondoka kwangu! Nayo, utakayonitoza, basi, nitayachukua, nikupe. Naye mfalme wa Asuri akambandikia Hizikia, mfalme wa Wayuda, kutoa vipande 300 vya fedha, ndio shilingi milioni tatu na nusu na vipande 30 vya dhahabu, ndio shilingi milioni sita na nusu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Hezekia, mfalme wa Yuda, akapeleka wajumbe waende Lakishi kwa mfalme wa Ashuru, kusema, Nimekosa; uniache ukarudi kwako; cho chote utakachoweka juu yangu, nitakichukua. Mfalme wa Ashuru akamtoza Hezekia, mfalme wa Yuda, talanta za fedha mia tatu, na talanta za dhahabu thelathini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia akatuma ujumbe kwa Saniharibu kule Lakisi na kumwambia: “Nimefanya makosa. Tafazali, uache kunishambulia, nami nitalipa chochote unachotaka.” Mufalme wa Asuria akaagiza Hezekia amuletee kilo elfu kumi za feza na kilo elfu moja ya zahabu.