2 Kings 18:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu, amiri mkuu, mkuu wa matowashi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi kwenda kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Walisafiri na kufika Yerusalemu. Nao walipowasili waliingia na kusimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea Uwanda wa Dobi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi, pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja Yerusalemu na kusimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na amiri wake
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu, amiri mkuu, mkuu wa matowashi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi kwenda kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Walisafiri na kufika Yerusalemu. Nao walipowasili waliingia na kusimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea Uwanda wa Dobi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi lake pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi mpaka kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja mpaka Yerusalemu na kusimama kando ya mfereji unaopeleka maji katika Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi, pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja Yerusalemu na kusimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na kamanda wake, toka Lakishi, kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika, wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu, amiri mkuu, mkuu wa matowashi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi kwenda kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Walisafiri na kufika Yerusalemu. Nao walipowasili waliingia na kusimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea Uwanda wa Dobi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mfalme wa Asuri akamtuma mkuu wa vita na mkuu wa watumishi wa nyumbani na mkuu wa askari, watoke Lakisi kwenda Yerusalemu na kikosi kikubwa, wakaupandia, wakafika Yerusalemu. Walipokwisha kupanda na kufika wakasimama kwenye mfereji wa ziwa la juu katika barabara iendayo Shambani kwa dobi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na amiri wake, toka Lakishi, kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika, wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme wa Asuria alimutuma majemadari wakubwa watatu pamoja na kundi kubwa la waaskari kutoka Lakisi kwenda kwa mufalme Hezekia kule Yerusalema. Walisafiri na kufika Yerusalema. Nao walipofika waliingia na kusimama karibu na mufereji wa kisima kinachokuwa upande wa juu katika barabara kubwa inayoelekea kiwanja cha mufuaji wa nguo.