2 Kings 18:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia huyo jemadari mkuu, “Tafadhali, sema nasi kwa lugha ya Kiaramu, maana tunaielewa; usiseme nasi kwa lugha ya Kiebrania; kwa kuwa watu walioko ukutani wanasikiliza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania, watu walio juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa hao watu walio ukutani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia huyo jemadari mkuu, “Tafadhali, sema nasi kwa lugha ya Kiaramu, maana tunaielewa; usiseme nasi kwa lugha ya Kiebrania; kwa kuwa watu walioko ukutani wanasikiliza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Eliyakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa Kiaramu, kwa kuwa tunakielewa vizuri. Usiseme nasi kwa Kiebrania wakati hao watu walio juu ya ukuta wanasikia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule kamanda, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa hao watu walio ukutani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Eliakimu mwana wa Hilkia, Shebna na Yoa wakamwambia huyo jemadari mkuu, “Tafadhali, sema nasi kwa lugha ya Kiaramu, maana tunaielewa; usiseme nasi kwa lugha ya Kiebrania; kwa kuwa watu walioko ukutani wanasikiliza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Sebuna na Yoa walipomwambia mkuu wa askari: Sema Kishami na watumishi wako! Kwani tunakisikia; usiseme na sisi Kiyuda masikioni pa watu hawa walioko ukutani!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, na Shebna, na Yoa, wakamwambia yule amiri, Tafadhali, sema na watumishi wako kwa lugha ya Kiashuri; maana tunaifahamu; wala usiseme nasi kwa lugha ya Kiyahudi, masikioni mwa hao watu walio ukutani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, Sebuna na Yoa wakamujibu yule jemadari: “Tafazali, useme nasi kwa luga ya Kiaramea maana tunaielewa. Usiseme nasi kwa luga ya Kiebrania. Watu wanaokuwa juu ya ukuta wanasikia.”