2 Kings 18:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mpaka baadaye nitakapokuja na kuwapeleka mbali katika nchi kama hii yenu, nchi yenye nafaka na divai, nchi yenye mikate na mashamba ya mizabibu; nchi yenye mizeituni na asali, ili mpate kuishi, msije mkafa.’ Msimsikilize Hezekia anapowahadaa akisema, ‘Mwenyezi-Mungu atatuokoa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hadi nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima, sio mauti! “Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha asemapo, ‘Mwenyezi Mungu atatuokoa.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, Bwana atatuokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mpaka baadaye nitakapokuja na kuwapeleka mbali katika nchi kama hii yenu, nchi yenye nafaka na divai, nchi yenye mikate na mashamba ya mizabibu; nchi yenye mizeituni na asali, ili mpate kuishi, msije mkafa.’ Msimsikilize Hezekia anapowahadaa akisema, ‘Mwenyezi-Mungu atatuokoa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mpaka nitakapokuja na kuwapeleka kwenye nchi iliyo kama hii ya kwenu, nchi yenye nafaka na divai mpya, nchi ya mikate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima na sio mauti! “Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha wakati anaposema, ‘BWANA atatuokoa.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya mizeituni na asali. Chagueni uzima, sio mauti! “Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa anawapotosha asemapo, ‘ bwana atatuokoa.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, BWANA atatuokoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mpaka baadaye nitakapokuja na kuwapeleka mbali katika nchi kama hii yenu, nchi yenye nafaka na divai, nchi yenye mikate na mashamba ya mizabibu; nchi yenye mizeituni na asali, ili mpate kuishi, msije mkafa.’ Msimsikilize Hezekia anapowahadaa akisema, ‘Mwenyezi-Mungu atatuokoa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
mpaka nitakapokuja, niwachukue kuwapeleka katika nchi iliyo kama nchi yenu. Nayo ni nchi inayojaa ngano na pombe, ni nchi yenye vyakula na mizabibu, tena ni nchi yenye mafuta ya michekele na asali, mpate kuwapo, msife. Msimwitikie Hizikia! Kwani atawapoteza na kusema: Bwana atatuponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, BWANA atatuokoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mpaka nitakapokuja na kuwapeleka katika inchi kama hii yenu, inchi yenye ngano na divai, inchi yenye mukate na mashamba ya mizabibu, inchi yenye mizeituni na asali, kusudi mupate kuishi, nanyi hamutakufa. Musimusikilize Hezekia anapowadanganya akisema: Yawe atatuokoa.