2 Kings 18:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliharibu mahali pote pa juu pa kuabudia miungu ya uongo na kuvunja nguzo za kutambikia na za mungu Ashera. Kadhalika, alivunja nyoka wa shaba ambaye Mose alimtengeneza, aliyeitwa Nehushtani. Mpaka wakati huo, watu wa Israeli walikuwa wakiitambikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Musa aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo Waisraeli walikuwa wanaifukizia uvumba. (Ilikuwa ikiitwa Nehushtani).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliharibu mahali pote pa juu pa kuabudia miungu ya uongo na kuvunja nguzo za kutambikia na za mungu Ashera. Kadhalika, alivunja nyoka wa shaba ambaye Mose alimtengeneza, aliyeitwa Nehushtani. Mpaka wakati huo, watu wa Israeli walikuwa wakiitambikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Mose aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (nayo ilikuwa ikiitwa Nehushtani).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu, akazivunja sanamu, akakatakata nguzo za Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ya shaba Musa aliyotengeneza, kwa kuwa hadi siku hizo wana wa Israeli walikuwa wanaifukizia uvumba (ilikuwa ikiitwa Nehushtani).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliharibu mahali pote pa juu pa kuabudia miungu ya uongo na kuvunja nguzo za kutambikia na za mungu Ashera. Kadhalika, alivunja nyoka wa shaba ambaye Mose alimtengeneza, aliyeitwa Nehushtani. Mpaka wakati huo, watu wa Israeli walikuwa wakiitambikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yeye akayakomesha matambiko ya vilimani, akazivunja nguzo za mawe za kutambikia, navyo vinyago vya Ashera akavikatakata, nayo ile nyoka ya shaba, Mose aliyoitengeneza, akaipondaponda, kwani mpaka siku hizo wana wa Isiraeli walikuwa wakiivukizia na kuiita Nehustani (Kinyago cha Shaba).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliharibu nafasi zote za kuabudu miungu na kuvunja nguzo na kukata Ashera. Vilevile, alivunja nyoka ya shaba ambayo Musa alitengeneza, iliyoitwa Nehustani. Mpaka wakati ule, watu wa Israeli walikuwa wakiitambikia.