2 Kings 19:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu akamwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, unayekaa katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa, ni wewe tu uliye Mungu, unayetawala falme zote za ulimwengu. Wewe uliumba nchi na mbingu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Hezekia akamwomba Mwenyezi Mungu akisema: “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, unayeketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Hezekia akaomba mbele za Bwana, akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu akamwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, unayekaa katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa, ni wewe tu uliye Mungu, unayetawala falme zote za ulimwengu. Wewe uliumba nchi na mbingu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Hezekia akamwomba BWANA akisema: “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, uliyeketi kwenye kiti chako cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako, ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe ndiye uliyeumba mbingu na dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Hezekia akamwomba bwana akisema: “Ee bwana, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Hezekia akaomba mbele za BWANA, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu akamwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, unayekaa katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa, ni wewe tu uliye Mungu, unayetawala falme zote za ulimwengu. Wewe uliumba nchi na mbingu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha Hizikia akamlalamikia Bwana akisema: Bwana Mungu wa Isiraeli uyakaliaye Makerubi, wewe ndiwe Mungu peke yako wa nchi zote za kifalme, wewe ndiwe uliyezifanya mbingu na nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Hezekia akaomba mbele za BWANA, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akamwomba Yawe akisema: “Ee Yawe, Mungu wa Israeli, unayeikaa katika kiti cha kifalme juu ya makerubi, ni wewe tu unayekuwa Mungu, unayetawala falme zote za ulimwengu. Wewe uliumba dunia na mbingu.