2 Kings 19:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwatuma wajumbe wako umemkashifu Bwana, wewe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima mpaka kilele cha Lebanoni. Nimekata mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri; nimeingia mpaka ndani yake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupitia kwa wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimepanda juu ya vilele vya milima, vilele vya juu sana katika Lebanoni. Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, misunobari yake iliyo bora sana. Nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana, misitu yake iliyo mizuri sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa vinywa vya wajumbe wako umemshutumu Bwana, ukasema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani pa Lebanoni. Nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri; nami nitaingia ndani ya makazi yake yaliyo mbali sana, na msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuwatuma wajumbe wako umemkashifu Bwana, wewe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima mpaka kilele cha Lebanoni. Nimekata mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri; nimeingia mpaka ndani yake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kupitia kwa wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimepanda juu ya vilele vya milima, vilele vya juu sana katika Lebanoni. Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, misunobari yake mizuri; nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana, misitu yake iliyo mizuri sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupitia kwa wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimepanda juu ya vilele vya milima, vilele vya juu sana katika Lebanoni. Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, misunobari yake iliyo bora sana. Nimefikia sehemu zake zilizo mbali sana, misitu yake iliyo mizuri sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa vinywa vya wajumbe wako umemshutumu Bwana, ukasema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani pa Lebanoni. Nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misonobari yake mizuri; nami nitaingia ndani ya makazi yake yaliyo mbali sana, na msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwatuma wajumbe wako umemkashifu Bwana, wewe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima mpaka kilele cha Lebanoni. Nimekata mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri; nimeingia mpaka ndani yake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ndiye, uliyembeua vinywani mwa wajumbe wako ukisema: Kwa kuwa magari yangu ni mengi, nimepanda milimani juu huko ndani Libanoni, nikaikata miangati yake mirefu na mivinje yake iliyochaguliwa, nikafika kwake huko juu kileleni, msitu unakokuwa kama shamba lake la miti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa vinywa vya wajumbe wako umemshutumu Bwana, ukasema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani pa Lebanoni. Nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri; nami nitaingia ndani ya makazi yake yaliyo mbali sana, na msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umewatuma watumishi wako kuchekelea Yawe; wewe umesema: Kwa magari yangu mengi ya vita, nimefika juu kwenye vichwa vya milima, mpaka kwenye vichwa vya milima ya Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misunobari mizurimizuri. Nimevifikia vichwa vyake na ndani ya pori zake kubwa.