2 Kings 19:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika, wamekuwa kama mimea ya shambani, kama majani yasiyo na nguvu. Kama majani yaotayo juu ya paa; yakaukavyo kabla ya kukua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika, wamekuwa kama mimea ya shambani, kama majani yasiyo na nguvu. Kama majani yaotayo juu ya paa; yakaukavyo kabla ya kukua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wake, wakiwa wameishiwa nguvu, wamevunjika moyo na wameaibishwa. Wamekuwa kama mimea katika shamba, kama machipukizi mabichi mororo, kama majani yanayochipua kwenye paa la nyumba, yaliyokauka kabla hayajakua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika, wamekuwa kama mimea ya shambani, kama majani yasiyo na nguvu. Kama majani yaotayo juu ya paa; yakaukavyo kabla ya kukua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao waliokaa humo mikono yao ikawa mifupi, wakastuka, wakaingiwa na soni, wakawa kama mapalizi ya shambani au kama ndago za uwandani au kama majani yameayo juu ya kipaa au kama shamba linyaukalo pasipo kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufazaika, wamekuwa kama mimea ya shamba, kama majani changa, kama majani yanayoota juu ya paa, yanayokauka mbele ya kukomaa.