2 Kings 19:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya mfalme wa Waashuru: ‘Hataingia katika mji huu wala kuupiga mshale wala kuujia kwa ngao wala kuuzingira.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hataingia katika mji huu wala hatapiga mshale hapa. Hatakuja mbele yake akiwa na ngao, wala kupanga majeshi kuuzingira.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Bwana asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya mfalme wa Waashuru: ‘Hataingia katika mji huu wala kuupiga mshale wala kuujia kwa ngao wala kuuzingira.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyo BWANA kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hataingia katika mji huu wala kupiga mshale hapa. Hatakuja mbele yake akiwa na ngao, wala kuweka jeshi kuuzunguka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo bwana kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hataingia katika mji huu wala hatapiga mshale hapa. Hatakuja mbele yake akiwa na ngao, wala kupanga majeshi kuuzingira.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi BWANA asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya mfalme wa Waashuru: ‘Hataingia katika mji huu wala kuupiga mshale wala kuujia kwa ngao wala kuuzingira.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya mfalme wa Asuri: hatauingia mji huu, wala hatapiga humu mshale, wala hataukaribishia ngao, wala hataujengea boma la kuuzingia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi BWANA asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Yawe anasema hivi juu ya mufalme wa Asuria: Hataingia katika muji huu, wala kuupiga mushale, wala kuingia akishika ngao, wala hatalundika udongo kandokando yake apate kuubomoa.