2 Kings 19:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, usiku huo malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu laki moja. Kulipopambazuka watu wakaamka, hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usiku ule, malaika wa Mwenyezi Mungu akaenda, akawaua wanajeshi elfu mia moja na themanini na tano katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, usiku huo malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu laki moja. Kulipopambazuka watu wakaamka, hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usiku ule, malaika wa BWANA akatokea na kuwaua watu 185,000 katika kambi ya Waashuru. Askari waliosalia walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usiku ule, malaika wa bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa usiku huo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia moja themanini na tano elfu. Na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, usiku huo malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu laki moja. Kulipopambazuka watu wakaamka, hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa usiku uleule, ndipo, alipotokea malaika wa Bwana, akapiga makambini kwa Waasuri watu 185000. Walipoamka asubuhi wakawaona hao wote, ya kuwa wamekufa, ni mizoga tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, malaika wa Yawe aliingia ndani ya kambi ya Waasuria na kuwaua watu elfu mia moja makumi nane na watano. Kesho yake, wakati watu walipoamuka, waliona yale maiti yote.