2 Kings 19:37 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja wakati Senakeribu alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki mungu wake, wanawe wawili, Adrameleki na Sharezeri walimuua kwa upanga, halafu wakakimbilia nchini Ararati. Naye Esar-hadoni, mwanawe akatawala badala yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja wakati Senakeribu alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki mungu wake, wanawe wawili, Adrameleki na Sharezeri walimuua kwa upanga, halafu wakakimbilia nchini Ararati. Naye Esar-hadoni, mwanawe akatawala badala yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja, wakati alipokuwa anaabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamwua kwa upanga, nao wakatoroka kwenda katika nchi ya Ararati. Esar-Hadoni mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja wakati Senakeribu alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki mungu wake, wanawe wawili, Adrameleki na Sharezeri walimuua kwa upanga, halafu wakakimbilia nchini Ararati. Naye Esar-hadoni, mwanawe akatawala badala yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, alipoomba nyumbani mwa mungu wake Nisiroki, ndipo, wanawe Adarameleki na Sareseri walipompiga kwa upanga, kisha wakaikimbilia nchi ya Ararati, naye mwanawe Esari-Hadoni akawa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja wakati Saniharibu alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisiroki mungu wake, wana wake wawili, Adarameleki na Sarezeri walimwua kwa upanga, halafu wakakimbilia katika inchi ya Ararati. Halafu mwana wake Esari-Hadoni akatawala kwa pahali pake.