2 Kings 19:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inawezekana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya jemadari mkuu, ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakaripia maneno aliyosikia. Kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yamkini Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya amiri huyu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inawezekana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya jemadari mkuu, ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakaripia maneno aliyosikia. Kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Inawezekana kuwa BWANA Mungu wako atasikia maneno yote ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai na kwamba atamkemea kwa maneno ambayo BWANA Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wanaishi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yamkini bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya kamanda huyu, ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA, Mungu wako; kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inawezekana Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya jemadari mkuu, ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai; naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakaripia maneno aliyosikia. Kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Labda Bwana Mungu wako ameyasikia yale maneno yote ya mkuu wa askari, ambayo bwana wake, mfalme wa Asuri, alimtuma kumbeua Mungu Mwenye uzima kwa kuyasema; Bwana Mungu wako na ampatilizie yale maneno, aliyoyasikia! Nawe na uje kuwaombea waliosalia walioko bado!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno yote ya amiri huyu, ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; naye atayakemea hayo maneno aliyoyasikia BWANA, Mungu wako; kwa sababu hii inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda Yawe, Mungu wako, alisikia maneno ya yule jemadari ambaye ametumwa na bwana wake mufalme wa Asuria, kwa kumutukana Mungu Mwenye Uzima, naye Yawe, Mungu wako atamwazibu kwa ajili ya maneno aliyosikia. Uwaombee watu wanaobaki.’ ”