2 Kings 2:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikawa wakati ulipofika ambapo Mwenyezi-Mungu alitaka kumchukua Elia mbinguni katika upepo wa kisulisuli, Elia na Elisha walikuwa njiani, wakitoka Gilgali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu alipokuwa karibu kumchukua Ilya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Ilya na Al-Yasa walikuwa njiani wakitoka Gilgali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, hapo Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikawa wakati ulipofika ambapo Mwenyezi-Mungu alitaka kumchukua Elia mbinguni katika upepo wa kisulisuli, Elia na Elisha walikuwa njiani, wakitoka Gilgali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati BWANA alipokuwa karibu kumchukua Eliya juu mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya na Elisha walikuwa njiani kutoka Gilgali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati bwana alipokuwa karibu kumchukua Ilya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Ilya na Al-Yasa walikuwa njiani wakitoka Gilgali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, hapo BWANA alipokuwa karibu kumchukua Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikawa wakati ulipofika ambapo Mwenyezi-Mungu alitaka kumchukua Elia mbinguni katika upepo wa kisulisuli, Elia na Elisha walikuwa njiani, wakitoka Gilgali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana alipotaka kumpaza Elia mbinguni kwa nguvu za upepo wenye ngurumo, Elia na Elisa walikuwa wakienda njiani kutoka Gilgali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, hapo BWANA alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ulifika ambapo Yawe alitaka kumupandisha Elia mbinguni katika upepo wa kuzungukazunguka. Elia na Elisha walikuwa katika njia, wakitoka Gilgali.