2 Kings 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akayapiga maji kwa vazi la Elia akisema, “Yuko wapi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Elia?” Alipoyapiga maji, yakagawanyika sehemu mbili, naye akavuka hadi ngambo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Ilya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ilya?” Al-Yasa alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akayapiga maji kwa vazi la Elia akisema, “Yuko wapi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Elia?” Alipoyapiga maji, yakagawanyika sehemu mbili, naye akavuka hadi ng'ambo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Eliya naye akayapiga nalo yale maji. Akauliza, “Yuko wapi sasa BWANA, Mungu wa Eliya?” Alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Ilya, naye akayapiga yale maji nalo. Akauliza, “Yuko wapi sasa bwana, Mungu wa Ilya?” Al-Yasa alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi BWANA, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akayapiga maji kwa vazi la Elia akisema, “Yuko wapi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Elia?” Alipoyapiga maji, yakagawanyika sehemu mbili, naye akavuka hadi ngambo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akalishika hilo joho la Elia lililokuwa limeanguka, akalipigisha maji akisema: Bwana Mungu wa Elia yuko wapi? Basi; hapo, yeye naye alipoyapiga maji, mara maji yakagawanyika huku na huko, naye Elisa akapita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi BWANA, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akayapiga maji kwa nguo ya Elia akisema: “Yuko wapi Yawe, Mungu wa Elia?” Alipopiga maji, yakagawanyika sehemu mbili, naye akavuka mpaka ngambo.