2 Kings 2:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanafunzi wa manabii kutoka Yeriko walipomwona, walisema, “Roho ya Elia iko kwa Elisha.” Basi, wakaenda kumlaki, wakasujudu mbele yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wana wa manabii kutoka Yeriko waliokuwa wakitazama wakasema, “Roho ya Ilya inamkalia Al-Yasa.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi chini mbele yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanafunzi wa manabii kutoka Yeriko walipomwona, walisema, “Roho ya Elia iko kwa Elisha.” Basi, wakaenda kumlaki, wakasujudu mbele yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wana wa manabii kutoka Yeriko, waliokuwa wakitazama, wakasema, “Roho wa Eliya inamkalia Elisha.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi nchi mbele yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wana wa manabii kutoka Yeriko waliokuwa wakitazama wakasema, “Roho wa Ilya inamkalia Al-Yasa.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi nchi mbele yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanafunzi wa manabii kutoka Yeriko walipomwona, walisema, “Roho ya Elia iko kwa Elisha.” Basi, wakaenda kumlaki, wakasujudu mbele yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi wa wafumbuaji waliokuwako Yeriko ng'ambo ya huku walipomwona wakasema: Roho yake Elia inamkalia Elisa. Wakamwendea, wakamwangukia chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona, walisema, Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanafunzi wa manabii kutoka Yeriko walipomwona, walisema: “Roho wa Elia yuko kwa Elisha.” Basi, wakaenda kumupokea, wakainama mbele yake kwa heshima.