2 Kings 2:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamwambia, “Sisi watumishi wako tunao mashujaa hamsini; tafadhali waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Ikiwa roho ya Mwenyezi-Mungu imembeba na kumtupa juu ya mlima fulani au bondeni.” Elisha akajibu, “La, msiwatume.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa Mwenyezi Mungu amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.” Al-Yasa akajibu, “Hapana, msiwatume.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda roho ya Bwana imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamwambia, “Sisi watumishi wako tunao mashujaa hamsini; tafadhali waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Ikiwa roho ya Mwenyezi-Mungu imembeba na kumtupa juu ya mlima fulani au bondeni.” Elisha akajibu, “La, msiwatume.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa BWANA amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.” Elisha akajibu, “Hapana, msiwatume.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho wa bwana amemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.” Al-Yasa akajibu, “Hapana, msiwatume.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda Roho ya BWANA imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamwambia, “Sisi watumishi wako tunao mashujaa hamsini; tafadhali waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Ikiwa roho ya Mwenyezi-Mungu imembeba na kumtupa juu ya mlima fulani au bondeni.” Elisha akajibu, “La, msiwatume.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia: Tazama, huku wako watu hamsini wenye nguvu; acha, tuwatume, waende kumtafuta bwana wako! Labda roho ya Bwana imemchukua, ikamweka juu ya mlima mmoja au katika bonde moja. Akawaambia: Msiwatume!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda roho ya BWANA imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamwambia: “Sisi watumishi wako tuko na mashujaa makumi tano. Tafazali, uwaruhusu waende kumutafuta bwana wako. Labda roho wa Yawe amemubeba na kumutupa juu ya mulima fulani au katika bonde.” Elisha akajibu: “Hapana, musiwatume.”