2 Kings 2:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye watu wa Yeriko walimwendea Elisha, wakamwambia, “Bwana, kama uonavyo mji huu ni mzuri, lakini maji tuliyo nayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa mji wakamwambia Al-Yasa, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu anavyoona, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haina mazao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye watu wa Yeriko walimwendea Elisha, wakamwambia, “Bwana, kama uonavyo mji huu ni mzuri, lakini maji tuliyo nayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa mji wakamwambia Elisha, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake ni mabaya na nchi haizai.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa mji wakamwambia Al-Yasa, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake ni mabaya, na nchi haizai.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye watu wa Yeriko walimwendea Elisha, wakamwambia, “Bwana, kama uonavyo mji huu ni mzuri, lakini maji tuliyo nayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watu wa huo mji wakamwambia Elisa: Tazama, hapa, mji huu unapokaa, ni pema, kama wewe bwana unavyoona, lakini maji ni mabaya, kwa hiyo nchi hii hupoozesha mimba, ziharibike.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha watu wa Yeriko wakamwendea Elisha, wakamwambia: “Bwana, kama vile unavyoona, muji huu ni muzuri, lakini maji tunayokuwa nayo ni mabaya na yanasababisha mimba kuharibika.”