2 Kings 2:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wa manabii waliokuwa huko wakamwendea Elisha, wakamwuliza, “Je, unajua kwamba leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa manabii waliokuwa Betheli wakamjia Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mwenyezi Mungu atakuondolea bwana wako leo?” Al-Yasa akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze kuhusu jambo hilo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elisha akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wa manabii waliokuwa huko wakamwendea Elisha, wakamwuliza, “Je, unajua kwamba leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa manabii walikuwako huko Betheli wakamjia Elisha na kumwuliza, “Je, unajua ya kwamba BWANA atakuondolea bwana wako leo?” Elisha akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa manabii waliokuwako huko Betheli wakamjia Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba bwana atakuondolea bwana wako leo?” Al-Yasa akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elisha akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wa manabii waliokuwa huko wakamwendea Elisha, wakamwuliza, “Je, unajua kwamba leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wanafunzi wa wafumbuaji waliomo Beteli walipomtokea Elisa, wakamwambia: Unajua, ya kuwa leo Bwana atamwondoa bwana wako kichwani pako? Akasema: Nami nayajua, nyamazeni tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elisha akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wa manabii wa Beteli wakamwendea Elisha, wakamwuliza: “Unajua kwamba leo Yawe atamupeleka bwana wako?” Elisha akajibu: “Ndiyo. Ninajua. Munyamaze.”