2 Kings 2:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende Yeriko.” Lakini Elisha akakataa akisema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja mpaka Yeriko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Ilya akamwambia, “Baki hapa, Al-Yasa. Mwenyezi Mungu amenituma Yeriko.” Naye akajibu, “Kwa hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana Bwana amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende Yeriko.” Lakini Elisha akakataa akisema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja mpaka Yeriko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Eliya akamwambia, “Baki hapa Elisha, BWANA amenituma Yeriko.” Naye akajibu, “Kwa hakika kama BWANA aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Ilya akamwambia, “Baki hapa, Al-Yasa. bwana amenituma Yeriko.” Naye akajibu, “Kwa hakika kama bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana BWANA amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende Yeriko.” Lakini Elisha akakataa akisema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja mpaka Yeriko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elia akamwambia: Elisa, kaa hapa! Kwani Bwana amenituma kwenda Yeriko. Akajibu: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa. Wakaja Yeriko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana BWANA amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Elia akamwambia Elisha: “Tafazali ubakie hapa. Yawe amenituma niende Yeriko.” Lakini Elisha akakataa akisema: “Kama vile Yawe anavyoishi na kama vile unavyoishi, sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja mpaka Yeriko.