2 Kings 2:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wa manabii huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumwuliza, “Je, unajua kwamba hivi leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akawajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa manabii waliokuwa Yeriko wakamwendea Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mwenyezi Mungu atakuondolea bwana wako leo?” Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wa manabii huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumwuliza, “Je, unajua kwamba hivi leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akawajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumwuliza, “Je, unajua ya kwamba BWANA atakuondolea bwana wako leo?” Akawajibu “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Al-Yasa na kumuuliza, “Je, unajua ya kwamba bwana atakuondolea bwana wako leo?” Akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wa manabii huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumwuliza, “Je, unajua kwamba hivi leo Mwenyezi-Mungu atamchukua bwana wako?” Elisha akawajibu, “Naam! Najua; nyamazeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wanafunzi wa wafumbuaji waliomo Yeriko walipomjia Elisa, wakamwambia: Unajua, ya kuwa leo Bwana atamwondoa bwana wako kichwani pako? Akasema: Nami nayajua, nyamazeni tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wa manabii wa Yeriko wakamwendea Elisha, wakamwuliza: “Unajua kwamba leo Yawe atamupeleka bwana wako?” Elisha akawajibu: “Ndiyo. Ninajua. Munyamaze.”