2 Kings 2:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali wewe kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende mtoni Yordani.” Lakini Elisha akasema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Ilya akamwambia, “Kaa hapa. Mwenyezi Mungu amenituma kwenda Yordani.” Naye akamjibu, “Kwa hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali wewe kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende mtoni Yordani.” Lakini Elisha akasema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa, BWANA amenituma kwenda Yordani.” Naye akamjibu, “Kwa hakika kama BWANA aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Ilya akamwambia, “Kaa hapa. bwana amenituma kwenda Yordani.” Naye akamjibu, “Kwa hakika kama bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Elia akamwambia Elisha, “Tafadhali wewe kaa hapa; Mwenyezi-Mungu amenituma niende mtoni Yordani.” Lakini Elisha akasema, “Naapa kwamba kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe mwenyewe uishivyo sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elia akamwambia: Kaa hapa! Kwani Bwana amenituma kwenda Yordani. Akajibu: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa. Wakaenda wote wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Elia akamwambia Elisha: “Tafazali ubakie hapa. Yawe amenituma niende Yordani.” Lakini Elisha akasema: “Kama vile Yawe anavyoishi na kama vile unavyoishi, sitakuacha.” Basi, wakaenda pamoja.