2 Kings 2:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elia akalivua vazi lake, akalikunja na kuyapiga maji, maji yakagawanyika katika sehemu mbili, nao wakavuka hadi ngambo ya pili, wakapitia mahali pakavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilya akatoa vazi lake, akalikunja na kupiga maji nalo. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elia akalivua vazi lake, akalikunja na kuyapiga maji, maji yakagawanyika katika sehemu mbili, nao wakavuka hadi ng'ambo ya pili, wakapitia mahali pakavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Eliya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elia akalivua vazi lake, akalikunja na kuyapiga maji, maji yakagawanyika katika sehemu mbili, nao wakavuka hadi ngambo ya pili, wakapitia mahali pakavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Elia alipolishika joho lake, akalizinga, akalipigisha maji; ndipo, yalipogawanyika huku na huko, nao wote wawili wakapita pakavu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elia akavua nguo yake, akaikunja na kupiga nayo maji. Maji yakagawanyika katika sehemu mbili, nao wakavuka mpaka ngambo, wakipitia pahali pakavu.