2 Kings 2:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika ngambo, Elia akamwambia Elisha, “Niambie unalotaka nikufanyie kabla sijaondolewa kwako.” Elisha akamwambia, “Naomba sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokwisha kuvuka, Ilya akamwambia Al-Yasa, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?” Al-Yasa akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika ng'ambo, Elia akamwambia Elisha, “Niambie unalotaka nikufanyie kabla sijaondolewa kwako.” Elisha akamwambia, “Naomba sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?” Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwisha kuvuka, Ilya akamwambia Al-Yasa, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?” Al-Yasa akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lolote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika ngambo, Elia akamwambia Elisha, “Niambie unalotaka nikufanyie kabla sijaondolewa kwako.” Elisha akamwambia, “Naomba sehemu maradufu ya roho yako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha pita, Elia akamwambia Elisa: Omba unayoyataka, nikufanyizie, nikiwa sijaondolewa kwako! Elisa akasema: Ninataka, mafungu mawili ya roho yako yaje kunikalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika ngambo, Elia akamwambia Elisha: “Uniambie jambo unalotaka nikufanyie mbele sijaondolewa kwako.” Elisha akamwambia: “Ninaomba sehemu mara mbili ya roho yako.”