2 Kings 20:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babuloni alisikia kuwa Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, akamtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo Merodak-baladani mwana wa Baladani, Mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana alipata habari kwamba Hezekia ameugua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babuloni alisikia kuwa Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, akamtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati ule Merodaki-Baladani mwana wa Baladoni mfalme wa Babeli akamtumia Hezekia barua pamoja na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo Merodak-baladani mwana wa Baladani, Mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana alipata habari kwamba Hezekia ameugua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babuloni alisikia kuwa Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, akamtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakati huo Berodaki-Beladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, akatuma barua na matunzo kwake Hizikia, kwani alisikia, ya kuwa Hizikia aliugua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo Merodak-baladani mwana wa Baladani, Mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana alipata habari kwamba Hezekia ameugua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, mufalme Berodaki-Baladana mwana wa Baladani mufalme wa Babeli alisikia kwamba Hezekia alikuwa amegonjwa na sasa amepona, alimutumia ujumbe pamoja na zawadi.