2 Kings 20:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hezekia akawakaribisha na kuwaonesha mali yake: Nyumba yake ya hazina, fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani na nyumba ya vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakukuwa chochote katika ikulu yake, au nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonesha vitu vyote vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina yake. Hapakuwa na kitu katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonesha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akawasikiliza, akawaonyesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonyesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hezekia akawakaribisha na kuwaonesha mali yake: nyumba yake ya hazina, fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani na nyumba ya vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakukuwa chochote katika ikulu yake, au nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake, yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu chochote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akawasikiliza, akawaonesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Hezekia akawakaribisha na kuwaonesha mali yake: Nyumba yake ya hazina, fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani na nyumba ya vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakukuwa chochote katika ikulu yake, au nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia akawasikiliza, akawaonyesha nyumba yote ya kuwekea mali zake, mlimo na fedha na dhahabu na manukato na mafuta mazuri, na nyumba ya mata yake nayo yote pia yaliyooneka katika vilimbiko vyake. Hakikuwako kitu, ambacho Hizikia hakuwaonyesha, wala nyumbani mwake, wala katika ufalme wake wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akawasikiliza, akawaonyesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonyesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hezekia akawakaribisha na kuwaonyesha mali yake: nyumba yake ya hazina, feza, zahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya bei kali na nyumba ya vifaa vyake vyote vya kiaskari na vitu vyote vilivyokuwa katika akiba zake. Hakukukuwa kitu chochote katika nyumba yake, au inchi yake ambacho hakuwaonyesha.