2 Kings 20:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kabla Isaya hajapita ua wa katikati, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia, kusema,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la Mwenyezi Mungu likamjia, akaambiwa:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kabla Isaya hajapita ua wa katikati, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia, kusema,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati neno la BWANA likamjia:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla Isaya hajaondoka katika ua wa kati, neno la bwana likamjia, akaambiwa:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, kabla Isaya hajatoka ua wa katikati ya mji, neno la BWANA likamjia, kusema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kabla Isaya hajapita ua wa katikati, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia, kusema,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Yesaya alipokuwa hajatokea mjini katikati, ndipo, neno la Bwana lilipomjia kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mbele Isaya hajapita kiwanja cha katikati, Yawe akamutolea ujumbe kusema: