2 Kings 20:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Rudi ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wa Mwenyezi-Mungu: Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu yako Daudi, nimesikia ombi lako na nimeona machozi yako. Nitakuponya na baada ya siku tatu utakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Rudi ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wa Mwenyezi-Mungu: Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu yako Daudi, nimesikia ombi lako na nimeona machozi yako. Nitakuponya na baada ya siku tatu utakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa baba yako Daudi, asemavyo: Nimeyasikia maombi yako na kuona machozi yako; nitakuponya. Katika siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekaluni mwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Rudi ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako; nitakuponya. Siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Rudi ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wa Mwenyezi-Mungu: Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu yako Daudi, nimesikia ombi lako na nimeona machozi yako. Nitakuponya na baada ya siku tatu utakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rudi kumwambia Hizikia aliye mkuu wao walio ukoo wangu: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa baba yako Dawidi anavyosema: Nimesikia kuomba kwako, nikayaona nayo machozi yako; na nikuponye, kesho kutwa upate kupanda kuingia Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Rudi umwambie Hezekia, mukubwa wa watu wa Yawe, na kumwambia: Mimi, Yawe, Mungu wa babu yako Daudi, nimesikia ombi lako na nimeona machozi yako. Nitakuponyesha na nyuma ya siku tatu utaenda katika nyumba ya Yawe.