2 Kings 21:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, licha ya dhambi yake alipowakosesha watu wa Yuda wakafanya dhambi kwa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Manase aliwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, damu ilijaa toka upande mmoja mpaka upande mwingine wa Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, licha ya dhambi yake alipowakosesha watu wa Yuda wakafanya dhambi kwa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Manase aliwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, damu ilijaa toka upande mmoja mpaka upande mwingine wa Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, hivyo kwamba wakatenda maovu machoni pa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, licha ya dhambi yake alipowakosesha watu wa Yuda wakafanya dhambi kwa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Manase aliwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, damu ilijaa toka upande mmoja mpaka upande mwingine wa Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Manase akazidi sana kumwaga damu za watu wasiokosa, akaujaza Yerusalemu hizo damu toka upande huu mpaka upande wa pili; tena kosa lake kubwa lilikuwa hilo la kuwakosesha Wayuda, wayafanye yaliyo mabaya machoni pake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya mambo hayo, Manase aliwaangusha watu wa Yuda katika zambi kwa kutenda maovu mbele ya Yawe. Aliwaua watu wengi wasiokuwa na kosa, damu ikajaa toka upande mumoja mpaka upande mwingine wa Yerusalema.