2 Kings 21:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matendo mengine ya Manase na yote aliyotenda, pamoja na dhambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matendo mengine ya Manase na yote aliyotenda, pamoja na dhambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha wafalme wa Yuda?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matendo mengine ya Manase na yote aliyotenda, pamoja na dhambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo mengine ya Manase nayo yote, aliyoyafanya, na makosa yake, aliyoyakosa, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wa Wayuda?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo mengine ya Manase na yote aliyofanya, pamoja na zambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Siku za Wafalme wa Yuda.