2 Kings 21:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye watumishi wa Amoni walikula njama na kumwua katika ikulu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watumishi wa Amoni wakampangia njama, nao wakamuua ndani ya jumba lake la kifalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye watumishi wa Amoni walikula njama na kumwua katika ikulu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wa Amoni wakafanya shauri baya dhidi yake, nao wakamwua mfalme katika jumba lake la kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watumishi wa Amoni wakamfitinia, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye watumishi wa Amoni walikula njama na kumwua katika ikulu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watumishi wa Amoni walipomlia njama, wakamwua mfalme nyumbani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha watumishi wa Amoni walimwasi na kumwua katika nyumba yake ya kifalme.